PATA KUJUWA SIRI YA MA GROUP YA WHATSAPP

magroup ya WhatsApp.
Kwanza kabisa tunaanza kwa kueleweshana neno la kingereza (Read by), maana ya hilo neno ni (Imesomwa na...).
Baada ya kuelewa hilo tuhamie hapa;
1. Najua unajua kuwa ukimtumia txt mtu ktk inbox/WhatsApp na akaisoma hupiga tiki mbili zenye rangi mkolezo.
2. Lakini ukituma ktk group hupiga tiki moja tu.
Sasa basi njia nyepesi kujua posti yako imesomwa na wangapi, unapaswa kufanya kifuatacho;
1. Anza kwa kuposti, posti yeyote ktk group lolote
2. Subiri hadi itakapo piga tiki moja
3. Upande huo huo wa tiki kwa maana ya upande wa kulia mwa posti yako, tumia kidole gumba kukandamiza kama unataka kuifuta, yaani kwa maana nyingine ikandamize moja kwa moja hadi option za kufuta, kuforward n.k zitokee
4. Option zikitokea relax kwanza, kisha katika hizo option angalia option yenye mduara ulio na herufi (i) katikati, hii inaitwa alama ya notification
5. Kama umeiona alama hiyo/mduara wenye herufi ai/(i) katikati basi ibonyeze
6. Sasa angalia hapo palipoandikwa "Read by" utaona list ya members ktk group hilo, na hao ndio waliosoma posti yako, tena utaona hadi muda halisi ambao kila member alipokuwa akisoma post yako
Nyongeza;
1. Kwa wale wenye magroup ya biashara, hapo utaweza kuona taarifa inafikia watu wangapi na kwa wakati gani.
2. Kwa wale mnaotumiana mabango ktk magroup, hapo utaweza kuona kama limemfikia muhusika.
3. Pia unaweza kukagua wangapi wapo Active, wangapi hawasomi kabisa, wangapi usoma posti yako usiku au baada ya siku nyingi, hivyo unaweza punguza mapuuza ktk magroup kwa njia ya kuangalia wasomaji

Comments