HEKAHEKA HEKAHEKA: Aishi na wanawake wawili chumba kimoja, alimdanganya mkewe ni dada yake




 December 8 2016 kupitia kipindi cha Leo   Fm Geah Habibu ametuletea Hekaheka inayotokea Dar es Salaam, Jamaa mmoja ambaye yeye anaishi na mkewe alimdanganya mkewe kwamba ana dada yake ambaye ana matatizo kwa hiyo akamuomba mkewe wakae naye pale nyumbani, mke wake alimkubalia lakini mke anasema akaona mambo hayaendi kama kweli ni mtu na dada yake.
Geah Habib aliongea na majirani ambao wamekuwa wakiamua ugomvi……>>>Walishagombana usiku tukaenda kuamua, yule mwanaume akaanza kujitetea kuwa yule alikuwa ni mwanamke wake wa mara ya kwanza kuna matatizo yalimtokea akamuomba mkewe waaishi naye akawa amekubali’-Jirani 
‘Tunalala kitandani mimi na mume wangu yule wifi yangu analala chini, nikishituka usingizini nakuta mume wangu amelala na dada yake chini, siku nyingine mume wangu ananituma dukani nikirudi nakuta wamefunga mlango nagonga mpaka wakija kufungua unaona tu jinsi ambavyo wametoka kufanya mapenzi’-Mke wa jamaa

Comments