
Maamuzi yaliofanywa katika kikao cha uendeshaji wa bodi ya Ligi imeamua kuwaondoa marefa Martin Saanya na Samwel Mpenzu katika ratiba ya uchezeshaji wa mechi za Ligi Kuu msimu wa 2016/2017 na kupelekwa katika kamati ya waamuzi ili suala lao lishughulikiwe kitaalam.
Hata hivyo kikao hicho pia kimemuondoa refa aliyechezesha mechi namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga Rajab Mrope na kumrudisha kwenye kamati ya waamuzi ili wampangie daraja lingine, Mrope amekutwa na hatia ya kosa la kutojihamini mchezoni.
Comments
Post a Comment