Yaya Toure: Mimi ni Mwislamu na sinywi pombe

Yaya Toure
Mchezaji nyota wa Ivory Coast Yaya Toure amesema hajapinga shtaka la 
kuendesha gari akiwa amelewa wiki mbili zilizopita.
Hata hivy alisema kwamba haunywa pombe    makusudi alipokamatwa akiendesha gari akiwa mlevi.
Ameandika kwenyeFACEBOOK kwamba "inafahamika wazi kwamba mimi ni Mwislamu na huwa sinywi pombe."
Hata hivyo, hajaelewa ni vipi alijipata akinywa pombe ama akajipata akiwa amelewa bila yeye kufahamu.
Mchezaji huyo wa Manchester City amesema: "Daima nimekuwa nikikataa pombe. Yeyote anayenifahamu na anayefuatilia uchezaji wangu atakuwa bila shaka ameniona nikikataa shampeni ya Mchezaji Bora wa Mechi kwa sababu ya kujitolea kwangu kuheshimu dini yangu."
"Ni muhimu kwangu kwamba niliiambia mahakama kwamba sikunywa pombe makusudi. Jaji akinihukumu mwenye alikubali kwamba sikuwa nimekunywa pombe makusudi."
Amesema kesi yake ilihitimishwa Jumatatu na kwamba alikubali shtaka.
"Kuendesha gari ukiwa mlevi ni kosa kubwa na ingawa sikunywa pombe makusudi, nakubali marufuku na faini na naomba radhi kwa yaliyotokea," aliongeza.

Comments